Mkristo Na Maisha Ya Maombi
Kitabu hiki kinatoa himizo kwa kila mkristo kwa habari ya umuhimu wa maombi. Maombi sio tuu ,kuomba ni suala la kimawasiliano kati ya mwanadamu na Mungu. Moja kati ya hasara kubwa kwa Mkristo ni kukaa bila mawasiliano na Mungu. Mahusiano hayawezi kudumu bila kuwa na muda kati ya wapenzi wawili ,vivyo hivyo huwezi kuhusiana na Mungu kama hauko tayari kumpa muda wako. Maombi ni zaidi ya mahitaji ,hatuombi ili kujibiwa mahitaji ,bali tunayatambua maombi kama sehemu ya kuimarisha ushirika kati yetu na Mungu. Kazi namba moja ya maombi sio kujibu mahitaji bali kubadili hali halisi ya muombaji ( tabia na mwenendo ili afananie na kile anachokiomba . Karibu sana katika safari hii ya kuanza kujifunza kuomba na kujua namna ya kuhusiana na Mungu wetu.
Read online + download
You might also like
Reviews
No reviews yet — be the first to read and review this book.